Wednesday, May 30, 2012

UPOTOSHAJI KTK MITANDAO YA KIJAMII



Kwanza nianze kwa kupongeza kuwepo kwa mitandao ya kijamii ambayo husaidia kupashana habari kwa haraka zaidi wakati wowote. Mitandao hii hii ndio iliyosaidia kuondoa viongozi wabovu madarakani na kuibua siri nyingi sana za nchi tofauti duniani kote.


Lakini mitandao hii siku za hivi karibuni imeanza kutumiwa isivyostahili, na watu wameigeuza kuwa vijiwe vya wahuni kutukanana, kujadiliana mambo binafsi yasiyoleta maendeleo katika jamii yetu. Mfano mzuri ni jamiiforums. Mtandao huu umesaidia sana kwa kuibua kashfa za ufisadi nchini Tanzania. Lakini pia ikumbukwe mtandao huu huu umegeuzwa kuwa wa chama kimoja specifically Chadema ( sina maana kwamba ni kitu kibaya, la hasha) na inapotokea mtu ukaisema vibaya chadema basi utaishia kutukanwa, kuitwa majina yasiyofaa na hali kadhalika. Na iwapo wewe ukawa mtu wa chama kingine na kutoa maneno ya kashfa kuhusu chadema basi jua utafungiwa (ban).


Sasa swali langu ni kwa nini jamiiforums inaibeba sana tabia ya "cyber bullying"  kupita kiasi ? Nafahamu kwamba mtandao huu ni "user generated content" lakini kwa nini uhalalishe hii tabia?  Kwa nini hawa wanachama wa Chadema wanatukana watu ovyo ovyo na kukashifu hata dini za watu ? Ndivyo wanavyofundishwa huko makao makuu yao ? Au hivi ndivyo Great Thinkers wanavyofikiri kama mnavyojiita? You guys need to grow up.


Ndugu zanguni, nia yangu si kuamsha hisia za chuki, ukabila au udini, bali ni kuelezea hali halisi iliyopo na inapaswa kuikemea tabia hii haraka.

Hapa chini ni sehemu ya ushahidi kutoka kwa mbunge aliyezushiwa habari ambazo si za kweli.
"Pamoja na Shukrani zangu kwa Waheshimiwa Wabunge,Mawaziri,na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana nami leo katika msiba ya marehemu Mama yangu... Nimeshitishwa sana na Uzushi uliosambazwa kwenye mtandao wa Jamii Forums kuwa Mke wangu na Baba yangu Mzazi nao wamefariki!... Kiukweli huu mtandao si tu unapoteza maana ya THE GREAT THINKERS bali unakuwa wa kihuni!..... Ni mtandao gani huu ambao hauwezi kuthibitisha taarifa kabla ya kuziandika public?...

Mtandao unaoandika uzushi wa kuzulia wengine vifo visivyokuwepo ni Mtandao wa ajabu!... Binafsi naomba kuwapa pole waliopata taarifa hizi (Wengine wameniandikia Inbox).. Naomba kuwajulisha kuwa Mke wangu na Baba yangu bado wanaendelea na Matibabu... Tuendelee kuwaombea wapone warejee kwenye majukumu yao kama kawaida!...

Nawatakia Usiku Mwema Ndugu zangu, Mungu awabariki.

Joseph Selasini
Mb. Rombo
Chadema."

Natumaini ujumbe huu utawafikia walengwa (Great Sinkers).



Blog yenu ya Makorokocho!

No comments: