Tuesday, June 26, 2012

BARAZA LA WAWAKILISHI ZNZ LIKIWA KAZINI


Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. Mohamed Aboud Mohamed kwa mwaka 2012/2013 katika Kikao cha Baraza hilo kinachoendela huko Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud akiwasilisha bajeti ya Wizara yake kwenye baraza la Wawakilishi jana
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar DR. Khalid Salum Mohd akiongoza jopo la watendaji waandamizi wa Wizara yake kufuatilia Hotuba ya Wizara yao Iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed katika Baraza la wawakilishi Zanzibar.
Watendaji wa Shirika l Utangazaji Zanzibar { ZBC } WAKIRUSHA HEWANI Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohamed Aboud Mohamed.Picha na Habari na Othman Khamis Ame-Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar.

Waziri wa Nchi na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame akiwa pamoja na Waziri wa Katiba na sheria wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ndani ya Baraza la Wawakilishi huko Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
Katibu wa Ofisi ya Mufti wa Zanzibar Sheikh Fadhil Soraga akibadilishana mawazo na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Mazrui nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Salmin Awadh Salmin kushoto akibadilishana Mawazo na Mwakilishi wa Kuteuliwa Asha Bakari nje ya Ukumbi Baraza la Wawakilishi huko Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.Picha na Yussuf Simai,Maelezo-Zanzibar

No comments: