Tumezama ktk jukwaa la Great Sinkers, aka vichwa vya panzi na panzi mmoja amekuja na hoja ya maana hapa chini.
Kuna kila njama zinazofanywa kwa makusudi kabisa, kupunguzia kasi Zitto Kabwe katika jukwaa la kisiasa. Njama hizo zinatokea kwa vigogo fulani wa CHADEMA, wanaomuona kuwa Zitto ni mwiba mkali.
Historia ya karibuni ilionesha kuwa Zitto alisakamwa sana alipotaka kugombea uenyekiti na baada ya kuzipangua hoja zote za kumuumiza kisiasa ndani ya CHADEMA akaambulia kupoozwa kwa kusukumiwa cheo cha unaibu Katibu Mkuu, cheo ambacho hakina manufaa yoyote kwa CHADEMA wala kwa Zitto. Ili kuponesha maumivu na kutibu majeraha ya kisiasa, Zitto akakikubali cheo hicho, lakini ukweli ni kwamba hakifanyii kazi yoyote.
Uthibitisho mwingine wa kumshusha kisiasa Zitto ni pale ambapo hajahudhuria vikao vya CHADEMA na Kikwete huko Ikulu, kuna mambo ya msingi ambayo Zitto amekuwa akitofautiana na viongozi wengine wa CHADEMA na hayo ndio yanamfanya ajaribiwe kushushwa hadi na kutokuwekwa kwenye maamuzi mengi ya chama na yeye hustukia tu maamuzi yameshafanywa. Na anapotoa misimamo yake huwa ina tofauti na ya chama chake, mifano ipo mingi.
Tunawaasa vigogo wa CHADEMA kuwa hata ndugu zetu wa Kigoma walipopiga kura za Ubunge zilikuwa ni kura za Zitto na si za CHADEMA, hilo walielewe. Kama ilivyo kwa kura za Shibuda, zilikuwa ni za Shibuda lakini si za CHADEMA hilo linajidhihiri kwa kuwa kura za Urais za Kigoma 90% zilikuwa za Kikwete hata kwenye jimbo la Zitto.
Aliposhindwa Mbowe uchaguzi mkuu wa 2005, 2010 akawekwa Slaa, tunataka Zitto agombee 2015 tumpe kura zetu, kumbuka, hatuwapi kura CHADEMA tutampa Zitto Kabwe, bila yeye sahauni kura za wengi.
Kati ya vitu asivyopendezwa navyo Zitto ni namna ya chaguzi za wabunge wa upendeleo zinavyoendeshwa kimabavu ndani ya CHADEMA.
Tunawatahadharisha CHADEMA wasimjaribu Zitto, wataumia kisiasa.
No comments:
Post a Comment