Tuesday, June 5, 2012
Shibuda wa Chadema aupania urais 2015
Mhe. John Maghale Shibuda Mbunge wa Maswa kwa Tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesikika mara kadhaa akijinadi yeye ni Rais ajae wa Tanzania kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema. Awali ilionekana kama anatania lakini leo tarehe 5.06.2012 akiwa ana changia katika kikao cha tisa cha Wadau wa Pamba kilichofanyika Chuo cha Benki Kuu Mjini Mwanza amesikika tena kwa msisitizo zaidi ya mara moja akiwataka wabunge, wakuu wa Mikoa na wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya wawe makini sana katika kusimamia zao la pamba nchini kwani kushindwa kwao kutakuwa ni tiketi ya kuanguka kwa Serikali ya CCM na kumpa fursa yeye kushinda wa Urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Kikao hicho kilichohudhuriwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya pamba nchini ikiwemo Wakuu wa Mikoa,Wakuu Wilaya, Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Wabunge wanaotoka mikoa inayolima pamba akiwemo Mhe. John Cheyo, Dr. Dalali Kafumu, Vincent Nyerere,Dk Charles Tizeba, Lembeli, Kingwangwala na wabunge wengine watokao maeneo ya kanda ya ziwa kilikuwa na mvutano mkali sana miongoni mwa wabunge hao hasa baada ya Mbunge wa Mwibara Kangi Lugola (CCM) kutoa kauli za kuwatuhumu wabunge wenzake kuwa na maslahi kwenye sekta ya pamba ambayo yanania ya kuwanyonya wakulima akiwamo Hamis Kingwangwala ambae ana kampuni ya ununuzi pamba lakini kwa wakati huo huo anadai kuwa anawatetea wakulima. Kauli ya Lugola ilimgusa pia Bw. Zizi ambae ni Mwenyekiti wa Chama cha wakulima wa Pamba (TACOGA) ambae nae anadaiwa kujihusisha na ununuzi wa pamba wakati huo huo akidai kuwa yeye ni mkulima na ana simama maslahi ya wakulima..
Katika hali isiyo ya kawaida, Mhe. Shibuda ambae aliwahi kuungana na baadhi ya wabunge wenzake toka maeneo yanayolima pamba kuitaka Serikali kumchukulia hatua Mkurungenzi wa Bodi ya Pamba Bw. Maiko Mtunga kuhusika na matumizi mabaya ya bilioni 2 zilizotolewa ili kuwafidia wakulima kutokana na mdororo wa uchumi (stimulus package) kufuatia ripoti Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma chini ya uongozi wa Mhe. Cheyo ambayo ilipendekeza kuvunjwa kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Pamba na kuwachukulia hatua watendaji wake, leo ameonyesha kumhurumia kwa kiasi kikubwa Mkurugenzi wa Bodi hiyo kwa kile alichodai hajatendewa haki kwa kusimamishwa na Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika. Alieleza kuwa labda kauli yake Mkurugenzi huyo za kuwadhalau wadau ndio yamemponza na sio suala la upotevu wa kiasi hicho cha fedha ambacho kama ndivyo, basi ilipaswa hata mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhe. Dr. Festus Limbu nae asimamishwe.
Shibuda alisisitiza kuwa Mkurugenzi huyo ameonewa na kwamba Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) anapaswa tena kufanya ukaguzi makini (forensic audit) kwenye Bodi ya Pamba kabla ya Serikali kuchukua uamuzi wa kumsimamisha Bw. Mtunga au mtu yeyotekutokana na taarifa ambazo huenda hazina ukweli kuhusu suala linalohusishwa na Mkurugenzi Mkuu huyo wa Bodi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment