Thursday, May 31, 2012

Adolf Hitler na kitabu chake cha ''Mein Kampf"

Hiki ndio kitabu alichoandika Adolf Hitler kuhusu kuwaangamiza wayahudi. Kitabu kilichapishwa mwaka 1925 (toleo la kwanza) na toleo la pili lilichapwa mwaka uliofuata 1926. Maana halisi ya neno "Mein Kampf" kwa lugha ya kiingereza ni "My struggle au My battle".

Kitabu hiki kilihaririwa na Bernhard Stempfle. Inasemekana kwamba bwana Adolf Hitler alihofiwa kwamba wayahudi wangeshika madaraka makubwa sana duniani katika nyanja mbalimbali kama siasa na biashara. Katika hiki kitabu, Hitler aliainisha vitu viwili vilivyomchukiza sana katika maisha yake ambavyo ni Ukomunisti na Uyahudi.

Kutokana na mauzo ya kitabu hiki, aliweza kununua Mercedes Benz kipindi hicho akiwa jela. Ingawa aliweza kuuza kopi 240,000 mwishowe aliishia kuwa na deni 405,500 German Reichsmark ambayo alikuja kusamehewa mwaka 1933.

Baada ya vita, kopi zaidi ya milioni kumi zilikuwa zimeshauzwa ama kusambazwa nchini Ujerumani.

No comments: