Wednesday, May 30, 2012

IDD SIMBA afikishwa mahakamani

  Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa zamani, Idd Simba akiongozwa na askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana kujibu mashata 8 likiwemo la kula njama na, kughushi pamoja na kulitia hasara Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA zaidi ya Sh. milioni 300. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengeni watatu.
 Mmoja wa watuhumiwa katika kesi hiyo, Aliyekuwa Diwani wa Sinza, Salim Mwaking'nda akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana mchana.
 Wakili Said Hamad El-Maamry (kushoto) akizungumza na Idd Simba Mahakamani hapo.
--
Na Mwandishi Wetu
 
Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya awamu ya Pili, Idd Simba ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la UDA leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashata 8 likiwemo la kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na kulisababishia hasara Shirika hilo ya zaidi ya Sh. bilioni 2.3

 Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengine watatu ambao Mbali na Idd Simba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya UDA ,wengine ni Mkurugenzi Salim Mwaking’inda na Meneja Mkuu wa shirika hilo, Victor Milanzi wa shirika hilo ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Alex Mgongolwa na Said El Mamry ambapo upande wa Jamhuri unawakilishwa na wakili wa Taasisis ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,Ben Lincol.

Mbele ya Hakimu Mfawidhi Ilivin Mugeta , wakili Lincoln alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na makosa nane.Alidai kosa la kwanza ni la kula njama ambalo linamkabili Simba na Milanzi kuwa kati ya Septemba 2 mwaka 2009 jijini Dar es salaam walikula njama na watu wasiofahamika walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa ya mwaka 2007.
Shitaka la tatu ni la kuamisha fedha kinyume na kifungu cha 29 cha Sheria ya kupambana na Rushwa, kwamba Simba na Milanzi kwa tarehe hiyo Simba akiwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Milanzi akiwa Meneja Mkuu wa UDA,kwa pamoja walishirikiana kuamisha fedha kwa faida yao binafsi sh 320,000,000,ikiwa ni malipo ya awali na ni sehemu ya ya malipo ya hisa za UDA ambazo walizipokea wao binafsi kupitia nyadhifa zao .
washitakiwa wote wametimiza masharti ya dhamana wenzake.Kesi hiyo imeairishwa hadi Juni 28 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.

No comments: