Wednesday, May 30, 2012

Matukio mbalimbali kuhusiana na fujo za ZNZ











 Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
 Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
 Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.Picha na Yussuf Simai-Zanzibar. (Chanzo: hakingowi)
Askofu Mkuu wa Tanzania Dk.Costantino Mokiwa  akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Pili wa  Rais Mohammed Aboud, walipofika Ofisi hapo kwa ajili ya mazungumzo na Waziri kuhusiana na vurugu zilizoyokea wiki iliopita na kusababisha uharibifu na uvyunjaji wa makanisa katika sehemu mbalimbali na mali za baadhi ya wananchi kuharibiwa.kutokana na vurugu hiyo. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud, akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Makanisa Tanzania  ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Tanzania Dk. Mokiwa, uliofika Ofisini kwake kwa mazungumzo.mjini Zanzibar.
 Maaskofu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,akitowa maelezo kwa ujumbe huu ulipofika Ofisini kwake Vuga. 

Waandishi wakiwa katika harakati za kazi zao ili kuwahabarisha Wananchi mambo yaliokuwa yakizungumzwa katika mkutano huo (chanzo: Othman Mapara)
Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanzibar, kuhusiana na fujo zilizotokea juzi Zanzibar, kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali. 
Waziri Dk. Nchimbi  akisisitiza jambo katika Mkutano wake na Viongozi wa Dini  kuzungumzia Vurugu zilizotokea juzi katika mitaa ya mji wa Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema, akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kilimani.
Viongozi wa Jumuiya za Kiislam Zanzibar  wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza nao kuhusiana na matukio yaliotokea katika Visiwa vya Zanzibar.  
Viongozi wa Jumuiya  za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena  ikaharibu  Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.
Mwandishi wa habari wa Nipashe Mwinyi Sadala akiuliza swalim katika Mkutano huo.uliowashirikisha Viongozi wa Jumuiya za Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuziungumzia vyurugu hizo..
Mwandishi wa Redio HIT FM, Jacob, alipota fursa ya kuuliza, katika Mkutano huo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Nchimbi.    
Ofisa wa Ubalozi wa Marekani aliopo Zanzibar Jefferson Smith, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kurudisha hali ya Amani katika Mji wa Zanzibar bila ya kutokea madhara kwa Wananchi na kulipongeza kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuzungumza  nao, jinsi ya kuzuiya tatazo hili lisitokee tena.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZATI  Zanzibar Abdulsamad, amesema yeye amefarijika kwa ujio wa Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP,na amelitaka jeshi la Polisi kuzuiya fujo kama hizi zisitokea tena katika Visiwa vya Zanzibar ambavyo huzoretesha shughuli za Kitalii ikizingatiwa wakati huu ni msimu wa Utalii ikizingatiwa Zanzibar ni moja ya nchi zilizokuwa na Vivutio vya Utalii.  



SHEKH. Saleh Zam, akitowa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya za Kiislam Zanzibar baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. (chanzo: OthamanMapara)


No comments: