MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe amesema chama chake kitazuia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakati wa mkutano wa Bunge la Bajeti unachotarajiwa kuanza Juni 12.
Mbowe alisema kuwa watafanya hivyo hadi Serikali itakapotoa ufafanuzi kuhusu hatima ya wakazi wa Tandahimba waliochomewa mali zao wakati wakiandamana kuadai haki zao akieleza kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu ni suala lisilokubalika.
Alitoa kauli hiyo alipohutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Tarafa ya Mahuta wilayani Tandahimba mkoani Mtwara ambapo alidai kuwa vitendo hivyo vinavyofanywa na Serikali ya CCM ndivyo vilivyoisukuma Chadema kufanya oparesheni nchi nzima na kwamba lengo la chama chake ni kuchukua dola katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2015.
“Hili la korosho na vurugu zilizotokea hatuwezi kuliacha hivi hivi, Chadema tutazuia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Wizara ya Mambo ya Ndani, hadi hapo Serikali itakapotoa tamko la hatima ya watu waliochomewa mali zao. Tunataka polisi watueleze wale waliojihusisha na vitendo hivyo wapo wapi na wanafanywa nini?”alisema Mbowe akihoji..
Alisema kuanzia sasa chama hicho kitahakikisha waathirika wote wa vurugu zilizofanyika mwezi Aprili mwaka huu, wanalipwa fidia na Serikali kwa kuwa utafiti waliofanya unaonyesha kuwa vurugu hizo zilisababishwa na kufanywa na polisi.
“Serikali lazima itoea tamko, hatua gani wamechukuliwa watu waliochoma maduka ya wananchi na mali zao. Chadema haiwezi kukubali na mimi niko tayari kufunguliwa kesi zaidi za uchochezi na hata kufungwa jela, lakini sitaacha kuelimashi wananchi juu ya haki zao na ninawamba muunge mkono Chadema ichukue dola mwaka 2015 ili mpate ukombozi wa kweli,”alisema.
Mbowe ametoa msimamo huo wa chama ikiwa ni muda mfupi baada ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willbrod Slaa kueleza dhamira ya chama hicho kuwa ni kuhakikisha inawatetea kwa nguvu zote wakazi wa Tandahimba walioharibiwa mali zao na kwamba chama hicho kimemkabidhi jukumu hilo Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni .
Mbowe alisema Chadema hakipo kwa ajili ya kuwania udiwani na uenyekiti wa serikali za mitaa bali ni kuingia Ikulu kuongoza dola na kuleta utetezi wa kweli wa rasimali za watanznaia zikiwamo madini gesi na mafuta kuwanufaisha pia wakazi wa maeneo zinakotoka.
Alisema dhamira ya Chadema ni kuondoa serikali ya CCM katika uchaguzi wa 2015 na kuwataka wakazi wa mikoa ya kusini kutuyumbishwa na propaganda za udini,ukabila ukanda na kuwataka wakazi wote wa kusini kuchagua chama chenye mlengo wa kuwakomboa bila kujali ni chama gani.
“Hadi sasa mimi ninakesi tisa za uchochezi, sitanyamaza hata wakiniongezea nyingine, nitaendelea kusema ukweli kuhusu masuala ya ukombozi wa wananchi,wakitika wanifunge na hata nikifa wakati wa mapambano wanamageuzi wote wekeni maiti yangu pembeni songeni mbele,ukombozi utaletwa na wanawake na wanaume, ”alisemaMbowe.
Akizungumzia utitiri wa vyama vya siasa nchini alisema hiyo ni mbinu za CCM za kudhoofisha upinzani ambapo wanatumia mbinu ya wagawe watatawenye iliyotumiwa na wakoloni walipotawala bara la Afrika.
MAONI YANGU: Hawa people's power wana matatizo gani ?
No comments:
Post a Comment