Saturday, June 2, 2012

Maswali yaelekezwa kwa Chadema

Chadema hawa ndio wale waliopinga CCM kuanzisha matawi ya chama nje ya nchi, na ndio Chadema hawa hawa wiki iliyopita walifungua tawi la chama chao nchini Marekani. Kama kweli waliona ni kosa kwa CCM kufungua matawi nje ya nchi, iweje na wao wafungue ikiwa wanaamini ni kosa ?
Chadema hawa ndio wanaopinga matumizi makubwa ndani ya serikali mfano mzuri, mfano wa magari. Wanapinga serikali kutumia magari ya bei ya gharama, NA WAO HAPO HAPO hao hao Chadema wanatumia magari ya gharama kubwa sana.
Chadema hawa hawa ndio waliotoa kauli chafu na za fujo kumtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano asikanyage katika baadhi ya mikoa ambao wao wanaamini ina wafuasi wengi na iwapo atakanyaga atahitaji passport kwa maana kwamba hiyo mikoa ni nchi tofauti na Tanzania. Sheria haziruhusu mtu yoyote ndani ya nchi ulazima wa kusafiri na passport, iweje Chadema watake kupindisha sheria? Wao si ndio wanaoamini katika sheria? Mbona ndio wao wanaotaka kuzivunja hizo sheria ?
Chadema hao ndio wale waliotaka baadhi ya mikoa iweze kujitawala yenyewe (Kanda za Kaskazini) kwa kuwa zina rasilimali za kutosha kama jiji la Mwanza, Kigoma na kwingineko. Kwa kifupi wanataka kuigawanya Tanzania katika makundi. Rasilimali za Taifa zitatumika kunufaisha kila mtanzania na sio baadhi ya mikoa tu kama wanavyotaka wao na kusahau mikoa isiyo na rasilimali.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe baada ya kushuka kwenye gari la bei mbaya
Mwananchi mwenzangu naomba msaada tutani!
Viongozi wa CHADEMA waliwahi kutoa madai kwamba viongozi wa serikali iliyopo madarakani wanatumia magari ya bei mbaya sana, na ni gharama kubwa kuyahudumia, kwa maana ya vipuri, service na mafuta.
Sasa swali ninalouliza ambalo naomba Watanzania wenzangu na wadau wengine popote duniani mnisaidie kupata jibu.Je.,mbona sasa na wao (Chadema) wanatumia magari kama hayo hayo wanayodai ni gharama kubwa???

Mnaweza kumjibu kwa kutoa Maoni kupitia ukurasa huu, au moja kwa moja kwenda kwake kwa mawasiliano haya hapa:-

PO BOX 33699,
HARBOUR VIEW TOWERS,
SAMORA AVENUE,
DAE ES SALAAM,
TANZANIA.
TEL + 255 22 2129550/1
FAX + 255 22 2129552
 

No comments: