Wednesday, June 27, 2012

JIHADHARI NA HUU UTAPELI

Kutokana na Kupenda Kuchunguza Mambo hususani ya msingi sana. Niliona Tangazo la Kazi Kupitia moja ya Blogu za Hapa tanzania nilihisi lakini Sikupenda Kuhukumu bila Kuwa na ushahidi na ufahamu wa kutosha kuhusu hilo Swala.

Hilo tangazo lilikua ni La Kazi nikaomba baada ya hapo wakaniambia nitumie CV, na kujibiwa kuwa baada ya Siku Mbili za Kazi nitajibiwa. Niliomba hiyo nafasi wiki iliyopita na Jana Nikajibiwa na Huu hapa Chini Ndio Ujumbe niliotumiwa na Hao Wahuni wa Mtandaoni ..

Habari,

Ninayofuraha kukufahamisha kuwa ombi lako la kufanya kazi na Mercycorps Nicaragua(Central America) limekubaliwa,nimeambatanisha barua ya kukubaliwa ambayo utasaini panapohusika na kuirudisha kwetu.
Kwa mujibu wa sheria za immigration hapa Nicaragua,NGO inatakiwa kukuombea Visa/work permit ili uweze kuja hapa kuanza kazi,kwa sasa hakuna ubalozi wa Nicaragua hapo Tanzania.
Kama ambavyo nilikutaarifu hapo awali unatakiwa kutuma malipo kwa ajili ya kuprocess Visa/Work permit yako mapema kama ambavyo barua ya kukubaliwa kazi inavyojieleza ili kutoa muda mzuri kwa NGO kuprocess kwa wakati ambapo itachukua siku 4 za kazi kupata kibali hicho cha Visa/Work permit.

Sasa katika kurahisisha utumaji wa malipo hayo Management imeomba kutumia account ya mfanyakazi ambaye yeye ana account ambayo ni International Account ambayo benki yake pia inapatikana hapo nchini Tanzania,hii ni kwa sababu ya kurahisisha na kuondoa gharama za utumaji na ucheleweshaji wa kupata malipo kwa wakati.
Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kubadili hiyo dola $197 kuwa Tanzania shillings ambayo ni sawa na Tsh.315,200/- ,harafu utadeposit hiyo Tsh.315,200/- kwenye account ifuatayo;
Tafadhali nakuomba uscan na unitumie payslip/Deposit slip baada ya kufanya malipo kwa Sababu Management itaihitaji kwa sababu za kiofisi,

Bank Name: Stanbic Bank
Account Name: Jacob E.E
Account Number: 0140518946701
Visa Card Number: 4313321007132065

Regards
Lilian Kisanga
Project Manager
Mercycorps
Nicaragua

Kutokana na Ujumbe huo Niliingiwa na Wasiwasi Sana na kujiuliza vitu vifuatavyo: Iweje Swala la Kulipa pesa ya Visa/Work Permit niliambiwa ni USD 197 iweje sasa Nilipe kwa Tsh? Halafu pili Iweje Nilipe kwenye Account ya Mtu binafsi? Baada ya hapo Ikabidi nifuatilie kuhusu hii account ikanibidi niwasiliane na Stanbic Bank kwaajili ya Ufafanuzi zaidi na Ubalozi wa Marekani.Huu hapa Chini ni Ujumbe niliopokea Kutoka Benki ya Stanbic Bank.....unasomeka hivi
"
Habari ,
Unashauriwa kwamba kwa sasa usiweke hela yoyote kwenye hiyo akaunti ya Jacob E.E.
Salamu,
Patricia
"
Ndugu Zangu Huu Ni Utapeli Kwahiyo Msitume

No comments: