ZAIDI ya Nchi 11 zimethibitisha kushiriki Maonyesho 36 ya Kimataifa ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), yatakayofanyika Viwanja vya Mwalimu Nyerere (Sabasaba) barabara ya Kilwa, Dar es salaam.
Maonyesho hayo yanatarajiwa kufunguliwa Juni 28 mwaka huu wakati serikali ikiwa kwenye mchakato wa kumtafuta mgeni rasmi.Akizungumza na gazeti hili jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, Samuel Mvingira alisema mabanda yatakuwa wazi kuanzia Juni 28 mwaka huu hadi Julai 10.
Mvingira alizitaja baadhi ya nchi zitazoshiriki ni pamoja na wenyeji Tanzania,Kenya na India.Nyingine ni China,Pakistan, Syria na Afrika ya Kusini.
Alisema katika Maonyesho hayo, zaidi ya kampuni 435 kutoka nchi mbalimbali zimethibitisha kushiriki kwenye maonyesho hayo mwaka huu kati ya hizo, nyingine zinatoka kwenye nchi zilizothibisha kushiriki.
“Mpaka sasa kampuni za ndani zilizothibitisha kushiriki ni 1500, yakiwamo mashirika 64,Taasisi za Serikali 8 na Mashirika yanayojishughulisha na shughuli za ujasilimali 11,” alisema Mvingira.
Na Patricia Kimelemeta
Aliongeza kuwa mwaka huu kiingilio kitakuwa Sh2500 kwa wakubwa, wakati watoto watalipia Sh500 na kwamba siku ya Saba Saba yenyewe kiingilio kitaongezeka na kufikia Sh3,000 kwa wakubwa na watoto Sh1000.
Alisema,kutokana na hali hiyo wanaamini kuwa ushiriki wa mwaka huu utakuwa mkubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita, kwa sababu wafanyabiashara wa nje wamejitokeza kwa wingi zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita.
“Kuna nchi zimeongezeka, na kwamba baadhi ya nchi zimewahi kushiriki kwenye maonyesho yaliyopita, na kwamba bado kuna baadhi ya nchi zinaendelea kuomba kushiriki,hivyo basi tunategemea nchi zitaongezeka,”aliongeza.
Maonyesho hayo mwaka jana yalifunguliwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal ambapo zaidi ya nchi 17 zilishiriki kwenye maonyesho hayo,huku makampuni 50 kutoka nje yalishiriki wakati makampuni ya ndani yalikuwa 1001.
No comments:
Post a Comment