Saturday, June 2, 2012

Taifa Stars wanacheza na Ivory Coast leo

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Kim Poulsen, ametaja kikosi cha cha kwanza kitakachoanza kuivaa Ivory Coast leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, katika mechi yake ya kwanza ya mchujo ya Kombe la Dunia.
Wachezaji wa timu ya soka ya Taifa, Kilimanjaro Taifa Stars wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho leo asubihi kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast. Kikosi hicho kinashuka dimabani leo kukabiliana na Ivory Coast.
Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Taifa Stars, Kim Poulsen, akizungumza na wachezaji wake baada ya kumalizika kwa mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast leo katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.
 
Kikosi kamili cha Taifa Stars ambayo itatumia mfumo wa 4-4-2 ni kima ifuatavyo;
Kipa; Juma Kaseja
Mabeki; Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris na Kevin Yondani
Viungo; Shabani Nditi, Salum Abubakari, Frank Domayo na Mwinyi Kazimoto
Washambuliaji; Mbwana Samata na Mrisho Ngasa
Wachezaji wa akiba; Mwadini Ali, Waziri Salum, Juma Nyoso, Erasto Nyoni, John Bocco, Simon Msuva, Jonas Mkude, Christopher Edward na Ramadhan Singano.
Kim amesema kikosi chake kimejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi hiyo, na kilichobaki ni kwa wachezaji kudhibitisha maandalizi hayo kwenye dakika 90 za mchezo huo utakaoanza saa 11 kamili jioni (nyumbani itakuwa saa 2 kamili usiku).
Mechi hiyo itaoneshwa moja kwa moja (live) kupitia televisheni ya RTI ambapo itaonekana katika nchi 58 duniani.
Mwamuzi; Slim Jedidi (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba 1; Bechir Hassani (Tunisia)
Mwamuzi msaidizi namba mbili; Sherif Hassan (Misri)
Mwamuzi wa akiba; Youssef Essrayri (Tunisia)
Mtathmini wa waamuzi; Rachid Medjiba (Algeria)
Kamishna wa mchezo; Saleh Issa Mahamat (Chad)
 
Kocha wa Makipa wa Kilimanjaro Taifa Stars, Juma Pondamali, akiwanoa makipa wa timu hiyo ikiwa ni hatua ya mwiso kabla ya kuvaana na Ivory Coast leo kwenye Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast.


Mshambuliaji Kilimanjaro Taifa Stars, Mbwana Samatta, akiweka saini kwenye madaftari ya vijana wa Ivory Coast baada ya kumaliza mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya mchujo ya kusaka tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ivory Coast katika Uwanja wa Felix Houphouet-Boigny jijini Abidjan, Ivory Coast. Samatta amekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wengi wa Ivory Coast.

No comments: