Wednesday, August 22, 2012

JUMUIYA YA WATANZANIA DC (DMV) KUFANYA PICNIC NA PARTY LA NGUVU 8/25/2012

Tanzania Community DMV with the Free good Food BBQ and more@ Regional Park 2000 Shorefield Road @ Wheaton, MD

And Same night is going down with the Full Disco Fiesta. NJOO ULISAGE RUMBA@ 4911 Prince Goerges Ave, Belsville MD 20705

From 9:PM UP2 2:AM, Kujaa Kulisakata Rumba
Get Your Summer Party with the Tanzania Community in DMV Full Disco Fiesta Patrieeeee is going on.!!








BREAKING NEWSSSS!!! MSANII DIAMOND KUELEKEA MAREKANI

Msanii wa Bongo Flavor Diamond kuelekea Marekani kwa kozi maalum.Pia kutumbuiza Washington DC. Habari zaidi, zikipatikana. Bongo flava inalipa kumbe.

UZUSHI UNAOSAMBAZWA NA WATU KUHUSU JUMUIYA YA UONGOZI WA WATANZANIA DMV

KUMEKUWA NA UZUSHI UNAOSAMBAZWA NA WATU WACHACHE ILI KUIBOMOA JUMUIYA YA WATANZANIA WASHINGTON DC, MARYLAND NA VIRGINIA. WATU HAO WANADAI KWAMBA UONGOZI UMEPOKEA RUSHWA KUTOKA CHAMA KIMOJA CHA SIASA CHENYE TAWI LAKE PALE DMV, WATU HAO PIA WAMESHINDWA KUJITAMBULISHA NA KUAMUA KUTUMIA MAJINA BANDIA KITU AMBACHO KINAWAFANYA WENGI WAAMINI WATU HAO HAWANA UHAKIKA AU HAWAJUI WANACHOONGEA. 

Tunataka kuwarahisishia watu hawa na madai yao, wanachotakiwa kufanya ni;

(a) Wajitambulishe ni akina nani.
(b) Waje na ushahidi wa madai yao.
(c) Ni sheria ipi ya katiba ya Jumuiya iliyovunjwa
AU WAKISHINDWA KUTHIBITISHA MADAI YAO
(d) Basi wakae kimya cuz they are full of sh*t, na waache jumuiy ifanye kazi na wapunguze chuki n porojo. Tuhuma hizi nig maneno tu hata kwenye kanga yapo.

NB. Toleo hili halijatolewa na uongozi wa Jumuiya na wala halihusiani na yoyote ndani ya uongozi.
NB. Blog hii haihusiki na ujumbe hapo juu.

Friday, August 17, 2012

WATANZANIA WA CHAMA KIMOJA CHA SIASA WASHINGTON DC WAANZISHA VITA YA MATUSI DHIDI YA CCM NA WATANZANIA WENZAO



KUNA UKURASA WA FACEBOOK PAGE ULIOFUNGULIWA NA WATANZANIA WANAOISHI HAPA DMV NA KUTUKANANA MATUSI MATUSI YA NGUONI NDANI YA MWEZI MTUKUFU HUU WA RAMADHANI.

Kuna page inaitwa XXXXXXXXXXXXXXX


Page hii inasemekana imefunguliwa na waTanzania wanaoishi hapa hapa Maryland wengine ni wavulana ambao wanajiita majina ya kike kutukana waTanzania wenye idikadi tafauti kwakuwa tu wanachuki binafsi na kuleta uhasama katika Jumuiya yetu, na wengine ni wasichana ambao nafsi zao zinavutwa na uhasama na chuki, pamoja nakujiingiza katika kundi ambalo hawastahili kuwemo alimradi tu wanafuata mkumbo na kusahau kuangalia malengo ya maisha yao kwa ujumla.

Chakushangaza wanajiita majina ya kiislamu na kutukana Matusi yanguoni ndani ya mwenzi huu wa Mtukufu wa Ramadhani, watu hao nina uhakika katika urafiki wa Facebook page zetu, tunao, na kule walipo wamejivalisha ngozi za nyoka kwa kubadili majina yao, katika mshuhuli mbali mbali ya kijumuiya pamoja na yakibinafsi, tunakuwa nao, chakushangaza zaidi wanadhani hawajulikani kumbe mitaani tayari wanajulikana juu ya hilo ila watu wanawaangalia mwishowao utafika wapi..?

Kumuweka mtu picha yake na kuanza kumtusi matusi yanguoni.

Hizi ni nafsi chafu ziliyojaa uadui uwovu na majivuno yakiambatana na kiburi na kutafuta kukomoana, pasipo sababu za maana. Hakuna tabia mbaya katika tabia za binadamu na yenye kuchukiwa kama tabia hizi ambazo katika jamii yetu sasa hivi zimetawala hata sijui watu hawa wamekusudia nini katika maisha yao ya baadae.

Kama tabia hizi zikiachiwa na kuendelea katika jumuiya yetu, zitamea kwenye nafsi zetu tutaanza kuondoa mfungamano wa kirafiki wa kindugu na hata majadiliano yetu hukosa busara na hikma kiasi cha kupelekea kwenye utengano na uhasama na chuki miongoni mwetu hapa.

Yote kutokana na utulivu wa nafsi, yanaotokana na tabia mbaya ya hasira ya kushindwa katika mihemko ya kutafuta maisha au kushindwa kwake katika kile unachokitafuta katika kuboresha maisha yake, kiasi ya kuvuruga mtiririko wa fikra chanya na kupelekea kuvuruga uthabiti wa kiroho juu ya mtu. Huenda ni kutokana na sababu Fulani fulani za kukosea hapa na pale au kujaribu hiki na kile, hamaki zake kupelekea kuwachukia wale waliojituliza kimaisha, kiasi ya kwamba kwa wale wasio na utulivu na uvumilivu uamua kuwasingizia mambo haya na yale wale wanao waona kuwa ni maadui zao.

Tabia hizi ni zawatu wachache tu walio katika kundi hili linaloitwa XXXXXXXXXXX limekuwa ni gumzo katika jamii yetu hapa DMV, kujihusisha katika Malimbano yaliokuwa si yalazima.

Nilijaribu kuingia katika kundi hilo na kutoa nasaha zilizobora pamoja na kuwakanya kuacha tabia hiyo mara moja, amaa sheria itafuata mkondo wake, matukeo yake niliambatia matusi na dada mmoja anajiita (Rukia Shabani) Na matokeo yake wakani toa katika kundi hilo, kuna baadhi ya watu ambao wamehusishwa katika kundi hilo wanafuatila kwa makini pamoja na kuwa Record zote tunazo na ushahidi wa baadhi ya watu waliotukanwa pamoja na maoni yao waliyatoa juu ya sakata hilo la matusi ya nguoni.

Tunajua Njia mojawapo ya kuishi kwa amani ni kuwa na utulivu wa moyo na kusahau mabaya ya watu hao huku tukizingatia umuhimu wa maisha yetu kwa kujaribu au kujitahidi kuishi kwa roho safi na huyapuuza mabaya na upinzani wa kiadui tunaokuta .

Hii ndio kazi yetu kutunza kumbukumbu juu ya yale yanayoendelea katika jamii yetu, hatutokaa kimyaa kuona uchafu kama huu unamea katika Jumuiya yetu na kudhalilishwa wengine ilimradi kufurahisha nafsi za watu wachache ambao tunauwezo wa kuwadhibiti.

Naomba mawazo na fikra zako tufanye nini ili tupunguze Uhasama na chuki zilizojaa ndani ya jumuiya yetu...?


chanzo ni mdau wetu wa marekani swahilivilla

Saturday, August 4, 2012

CCM YAFUTURISHA JIJINI WASHINGTON DC (DMV)

Saturday, August 4, 2012

Makada wa CCM wakiwa na kadi za uwanachama kwa wanachama wapya katika futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Mwenyekiti wa tawi la CCM DMV Loveness Mamuya akipata picha na tikiti maji lililochongwa kwa longo ya Chama cha CCM, katika futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Tikiti maji lililochongwa kwa longo ya Chama cha Mapenduzi CCM

Baadhi ya waTanzania mbali mbali waliohudhuria kwenye futari hiyo ilioandaliwa na tawi la CCM DMV

Baadhi ya waTanzania waliovalia rangi za chama cha CCM wakiwa kwenye futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV, Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.

Makada wa CCM Tawi la DMV shoto Mbunifu wa Ma Winny Casey Khanga Wrap Designer, pamoja na Peter Ligate (Picha ya kulia) wakiwa katika mpango mzima wa futari ya pamoja ilioandaliwa na wanatawi la CCM DMV

Watanzania waliojumuika kwenye futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV, Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.


Mwenyekiti wa tawi la CCM DMV Loveness Mamuya akiwakaribisha rasmi wageni walikwa kwenye futari ya pamoja ilioandaliwa na tawi la CCM DMV, Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani.


Baadhi ya wanachama wa CCM Tawi la DMV wakipata picha ya pamoja baada ya futari walioiyanda


Wanachama wa CCM Tawi la DMV na baadhi ya wageni wawili kutoka Londan Uingereza

Wageni wawili majirani wapendanao kutoka jijini London pia walihudhuria katika futari hiyo ilioandaliwa na ilioandaliwa na tawi la CCM DMV Jana Ijumaa Aug 3, 2012 katika ukumbi wa Hillandale Park iliyopo Silver Spring, Maryland Nchini Marekani

Katibu wa CCM DMV Jacob Kinyemi, kushoto akipata picha ya pamoja na Halima baada ya kumkabidhi rasmi kadi ya uwanachama wa CCM, Jana Ijumaa na kuwa mwanachama rasmi wa CCM.