Friday, August 17, 2012

WATANZANIA WA CHAMA KIMOJA CHA SIASA WASHINGTON DC WAANZISHA VITA YA MATUSI DHIDI YA CCM NA WATANZANIA WENZAO



KUNA UKURASA WA FACEBOOK PAGE ULIOFUNGULIWA NA WATANZANIA WANAOISHI HAPA DMV NA KUTUKANANA MATUSI MATUSI YA NGUONI NDANI YA MWEZI MTUKUFU HUU WA RAMADHANI.

Kuna page inaitwa XXXXXXXXXXXXXXX


Page hii inasemekana imefunguliwa na waTanzania wanaoishi hapa hapa Maryland wengine ni wavulana ambao wanajiita majina ya kike kutukana waTanzania wenye idikadi tafauti kwakuwa tu wanachuki binafsi na kuleta uhasama katika Jumuiya yetu, na wengine ni wasichana ambao nafsi zao zinavutwa na uhasama na chuki, pamoja nakujiingiza katika kundi ambalo hawastahili kuwemo alimradi tu wanafuata mkumbo na kusahau kuangalia malengo ya maisha yao kwa ujumla.

Chakushangaza wanajiita majina ya kiislamu na kutukana Matusi yanguoni ndani ya mwenzi huu wa Mtukufu wa Ramadhani, watu hao nina uhakika katika urafiki wa Facebook page zetu, tunao, na kule walipo wamejivalisha ngozi za nyoka kwa kubadili majina yao, katika mshuhuli mbali mbali ya kijumuiya pamoja na yakibinafsi, tunakuwa nao, chakushangaza zaidi wanadhani hawajulikani kumbe mitaani tayari wanajulikana juu ya hilo ila watu wanawaangalia mwishowao utafika wapi..?

Kumuweka mtu picha yake na kuanza kumtusi matusi yanguoni.

Hizi ni nafsi chafu ziliyojaa uadui uwovu na majivuno yakiambatana na kiburi na kutafuta kukomoana, pasipo sababu za maana. Hakuna tabia mbaya katika tabia za binadamu na yenye kuchukiwa kama tabia hizi ambazo katika jamii yetu sasa hivi zimetawala hata sijui watu hawa wamekusudia nini katika maisha yao ya baadae.

Kama tabia hizi zikiachiwa na kuendelea katika jumuiya yetu, zitamea kwenye nafsi zetu tutaanza kuondoa mfungamano wa kirafiki wa kindugu na hata majadiliano yetu hukosa busara na hikma kiasi cha kupelekea kwenye utengano na uhasama na chuki miongoni mwetu hapa.

Yote kutokana na utulivu wa nafsi, yanaotokana na tabia mbaya ya hasira ya kushindwa katika mihemko ya kutafuta maisha au kushindwa kwake katika kile unachokitafuta katika kuboresha maisha yake, kiasi ya kuvuruga mtiririko wa fikra chanya na kupelekea kuvuruga uthabiti wa kiroho juu ya mtu. Huenda ni kutokana na sababu Fulani fulani za kukosea hapa na pale au kujaribu hiki na kile, hamaki zake kupelekea kuwachukia wale waliojituliza kimaisha, kiasi ya kwamba kwa wale wasio na utulivu na uvumilivu uamua kuwasingizia mambo haya na yale wale wanao waona kuwa ni maadui zao.

Tabia hizi ni zawatu wachache tu walio katika kundi hili linaloitwa XXXXXXXXXXX limekuwa ni gumzo katika jamii yetu hapa DMV, kujihusisha katika Malimbano yaliokuwa si yalazima.

Nilijaribu kuingia katika kundi hilo na kutoa nasaha zilizobora pamoja na kuwakanya kuacha tabia hiyo mara moja, amaa sheria itafuata mkondo wake, matukeo yake niliambatia matusi na dada mmoja anajiita (Rukia Shabani) Na matokeo yake wakani toa katika kundi hilo, kuna baadhi ya watu ambao wamehusishwa katika kundi hilo wanafuatila kwa makini pamoja na kuwa Record zote tunazo na ushahidi wa baadhi ya watu waliotukanwa pamoja na maoni yao waliyatoa juu ya sakata hilo la matusi ya nguoni.

Tunajua Njia mojawapo ya kuishi kwa amani ni kuwa na utulivu wa moyo na kusahau mabaya ya watu hao huku tukizingatia umuhimu wa maisha yetu kwa kujaribu au kujitahidi kuishi kwa roho safi na huyapuuza mabaya na upinzani wa kiadui tunaokuta .

Hii ndio kazi yetu kutunza kumbukumbu juu ya yale yanayoendelea katika jamii yetu, hatutokaa kimyaa kuona uchafu kama huu unamea katika Jumuiya yetu na kudhalilishwa wengine ilimradi kufurahisha nafsi za watu wachache ambao tunauwezo wa kuwadhibiti.

Naomba mawazo na fikra zako tufanye nini ili tupunguze Uhasama na chuki zilizojaa ndani ya jumuiya yetu...?


chanzo ni mdau wetu wa marekani swahilivilla

No comments: