Thursday, May 31, 2012

Maandamano ya amani ya Chadema yapigwa stop

Mbunge wa Chadema Mh. Selasini aendelea vizuri

Vurugu za Zanzibar ktk Taarifa ya Habari

Mimi na Tanzania: Bi Saada

MUHIMU: Msaada wa Haraka Unahitajika


 Miguu ya NeemaHali ya Neema George inazidi kuzorota siku baada ya siku, miguu ikiwa imevimba, akitaabika katika suala la kula, kuongea na akipata maumivu makali ya tumbo hasa nyakati za usiku.
 Baba mzazi wa Neema, George Mugunga (kushoto) anasema kuwa mnamo mwaka 2010 mara baada ya hali ya mtoto wake kuzorota alimfikisha katika hospitali ya Rufaa Bugando kwaajili ya matibabu, lakini mara baada ya vipimo kufanyika vikaonyesha kuwa moyo wa mtoto wake una matundu matatu.
 Neema akiwa na mwandishi wa habari hizi Albert G. Sengo aliyefika nyumbani kwa bibi wa mtoto huyu eneo la Butimba mkoani Mwanza kwaajili ya kuchukuwa taarifa zaidi.Kutokana na kiwango kilichotamkwa kuwa kinahitajika kwa ajili ya tiba nje ya nchi, familia ya mtoto huyu ilikata tamaa  kabisa na kukata shauri la kumpeleka Sengerema kijijini ili akatibiwe na waganga wa kienyeji ndipo bwana Azizi Bukene (ambaye ni jirani yao) akashauri kuita vyombo vya habari kwaajili ya kulifikisha kwa umma kwa msaada.
Madaktari kupitia kliniki aliyokuwa akipata huduma (Bugando) wamesema kuwa tatizo la neema ni kubwa na haliwezi kupatiwa ufumbuzi hapa nchini bali linaweza kupata tiba Nchini India kwa makadirio ya gharama ya shilingi za kitanzania milioni 25.
 Pichani mtoto Neema George aliyegundulika kuwa na matundu matatu kwenye moyo.Mtoto Neema George (16) amewaomba wasamaria wema wajitokeze kumchangia fedha ili akapate matibabu ya moyo nchini India.
 Familia ya mtoto huyu inategemea kilimo kama sehemu ya kipato cha kuendesha maisha ya kila siku, hivyo uwezo wa kufikisha kiwango hicho cha fedha hata kupata matibabu kwa manufaa ya mtoto huyo kuendelee na masomo ni ndoto za alinacha.
Nje ya nyumba.

Wabunge wa Chadema walipoenda kuangalia soccer Brazil vs America

 Nabendera ya Taifa wakishangilia Bao la  kwanza la Brazil lilifungwa kwa Penalti na mchezaji Neymar
 Wabunge wa chama cha Chadema wakipata flash ya pamoja na warembo wa Kibrazil ndani ya uwanja wa FedexField, uliopo Landover Maryland Nchini marekani.
 Hivyo ndivyo ilivyo katika uwanja wa FedexFeild, uliopo Landover Maryland Nchini Marekani 
 Idadi ya wapenzi waliohudhuria katika mpambano huo ni 67,656 wakiwemo  Mhe. Nassari Joshua pamoja na Mhe, Peter Msigwa
 Picha ya pamoja na viongozi wa juu wa Chadema kwenye mpambano wa US na Brazil Usiku wa kuamkia leo  Alhamis Mei 31,2012 ndani ya ndani ya uwanja wa Fedex, uliopo Landover Maryland Nchini marekani
 Wachezaji wa Brazil wakilinda ngome yao kwa kuwadhibiti timu ya US kwenye mechi hiyo ya kirafiki ambapo timu ya Brazil waliweza kuwabamiza US bao 4-1 nyumbani kwao.
 US. hoi kwa Brazil baada ya kubamizwa bao nne bao la kwanza lilifungwa na Neymar, na lapili na Thiago mnamo wa dakika ya 11, kipindi cha kwanza. bao la US lilifungwa na Hercules Gomes dakika ya 44 kipindi chakwanza hadi mapumziko Brazil 2 US 1 kwenye mchezo wa kirafiki.
Wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe, Peter Msigwa na Mhe. Nassari Joshua, Al-Marufu Dogo janja, wakiwa na uwongozi wa tawi la Chadema Washington Dc Libe Mwangombe, wanne, Mjomba a.k.a Cosmas, Mzee wa swahilivilla Aboh Shatry wa pili kulia, pamoja na mashabiki wa US, wakiiunga mkono bendera ya taifa.
(chanzo: swahilivilla)

Kikwete ktk Mkutano Mkuu wa bodi ya magavana mjini Arusha

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31. 2012
 Ukumbi wa AICC wakati wa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua Mkutano wa Mkuu wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Africa afDB katika ukumbi wa AICC jijini Arusha leo Mei 31. 20
Rais Kikwete akiwa na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Rais Mstaafu wa Botswana Mh Festus Moghae, Rais wa Benki ya Africa Dkt Donald Kaberuka, Mshauri wa Mfalme wa Morroco Bw Omar Kabbaj (kushoto) , Waziri wa Fedha Dkt  William Mgimwa (wa pili kuhsoto) katika picha ya pamoja na Marais wastaafu wa Benki ya Afrika.Picha na IKULU

Adolf Hitler na kitabu chake cha ''Mein Kampf"

Hiki ndio kitabu alichoandika Adolf Hitler kuhusu kuwaangamiza wayahudi. Kitabu kilichapishwa mwaka 1925 (toleo la kwanza) na toleo la pili lilichapwa mwaka uliofuata 1926. Maana halisi ya neno "Mein Kampf" kwa lugha ya kiingereza ni "My struggle au My battle".

Kitabu hiki kilihaririwa na Bernhard Stempfle. Inasemekana kwamba bwana Adolf Hitler alihofiwa kwamba wayahudi wangeshika madaraka makubwa sana duniani katika nyanja mbalimbali kama siasa na biashara. Katika hiki kitabu, Hitler aliainisha vitu viwili vilivyomchukiza sana katika maisha yake ambavyo ni Ukomunisti na Uyahudi.

Kutokana na mauzo ya kitabu hiki, aliweza kununua Mercedes Benz kipindi hicho akiwa jela. Ingawa aliweza kuuza kopi 240,000 mwishowe aliishia kuwa na deni 405,500 German Reichsmark ambayo alikuja kusamehewa mwaka 1933.

Baada ya vita, kopi zaidi ya milioni kumi zilikuwa zimeshauzwa ama kusambazwa nchini Ujerumani.

Wednesday, May 30, 2012

Timu ya Taifa ya Soccer Zanzibar, Zanzibar Heroes ktk mazoezi

 Kocha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Hemed Suleiman Moroco, akitowa maelekezo kwa wachezaji wa timu hiyo katika mazoezi ya kujiandaa na michuano ya Kombe la Dunia kwa Nchi zilizokua sio Wanachama wa FIFA, wakiwa katika mazoezi uwanja wa Mao Dze Dong.   
 Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar wakijifua katika mazoezi uwanja wa Mao.

o Upelechanzo

Matukio mbalimbali kuhusiana na fujo za ZNZ











 Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud akielezea jambo kwa Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga wakwanza kulia kuhusiana na kuchomwa moto kwa Kanisa hilo liliopo Kariakoo Mjini Zanzibar katikati ni  Mkuu wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwemwa.
 Mku wa Jeshi la Polisi I,G,P Saidi Mwema akitoa hotuba kwa Maaskofu na baadhi ya waumini wa Kikristo katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar lililochomwa moto,ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.kuliani kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Abdalla Mwinyi na kushoto yake ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Mussa Ali Mussa.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Abdalla Mwinyi Khamis akitoa hotuba na kuonyesha Umoja na Mshikamano uliokuwepo kati ya Waislam na Wakristo kwa Picha ambayo imebuniwa na Mchoraji wa kingereza na kuwataka kuendelea na mshikamano wao ili kuzidi kuleta amani nchini.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akielezea  kwa Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud na Viongozi wengine mbalimbali kile kilichotokea baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.
 Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akibubujikwa na Machozi kwa kuguswa na hotuba iliokuwa ikitolewa na Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohd Aboud baada ya Kanisa hilo kuchomwa motokatika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tukio hilo.
 Mkuu wa Dini ya Kiislam Afisi ya Mufti wa Zanzibar Thabit Noman Jongo akitoa hotuba ya Dini inavyoeleza kuhusiana na kudumisha Amani na Usalama katika nchi na kuondosha mifarakano na chuki na kuharibu mali.Katika kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar ambalo limechomwa moto.
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Zanzibar Dickson D,Kaganga akimuonesha Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohd Aboud maeneo yalioathirika zaidi baada ya Kanisa hilo kuchomwa moto katika Vurugu zilizotokea Zanzibar ambapo hadi sasa watu 30 wamekamatwa  na baadhi yao kuhusishwa na tokeo hilo.Picha na Yussuf Simai-Zanzibar. (Chanzo: hakingowi)
Askofu Mkuu wa Tanzania Dk.Costantino Mokiwa  akizungumza na Waziri wa Nchi Ofisi yaMakamu wa Pili wa  Rais Mohammed Aboud, walipofika Ofisi hapo kwa ajili ya mazungumzo na Waziri kuhusiana na vurugu zilizoyokea wiki iliopita na kusababisha uharibifu na uvyunjaji wa makanisa katika sehemu mbalimbali na mali za baadhi ya wananchi kuharibiwa.kutokana na vurugu hiyo. 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Mohammed Aboud, akizungumza na Ujumbe wa Viongozi wa Makanisa Tanzania  ukiongozwa na Askofu Mkuu wa Tanzania Dk. Mokiwa, uliofika Ofisini kwake kwa mazungumzo.mjini Zanzibar.
 Maaskofu wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,akitowa maelezo kwa ujumbe huu ulipofika Ofisini kwake Vuga. 

Waandishi wakiwa katika harakati za kazi zao ili kuwahabarisha Wananchi mambo yaliokuwa yakizungumzwa katika mkutano huo (chanzo: Othman Mapara)
Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanzibar, kuhusiana na fujo zilizotokea juzi Zanzibar, kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali. 
Waziri Dk. Nchimbi  akisisitiza jambo katika Mkutano wake na Viongozi wa Dini  kuzungumzia Vurugu zilizotokea juzi katika mitaa ya mji wa Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema, akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kilimani.
Viongozi wa Jumuiya za Kiislam Zanzibar  wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza nao kuhusiana na matukio yaliotokea katika Visiwa vya Zanzibar.  
Viongozi wa Jumuiya  za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena  ikaharibu  Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.
Mwandishi wa habari wa Nipashe Mwinyi Sadala akiuliza swalim katika Mkutano huo.uliowashirikisha Viongozi wa Jumuiya za Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuziungumzia vyurugu hizo..
Mwandishi wa Redio HIT FM, Jacob, alipota fursa ya kuuliza, katika Mkutano huo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Nchimbi.    
Ofisa wa Ubalozi wa Marekani aliopo Zanzibar Jefferson Smith, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kurudisha hali ya Amani katika Mji wa Zanzibar bila ya kutokea madhara kwa Wananchi na kulipongeza kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuzungumza  nao, jinsi ya kuzuiya tatazo hili lisitokee tena.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZATI  Zanzibar Abdulsamad, amesema yeye amefarijika kwa ujio wa Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP,na amelitaka jeshi la Polisi kuzuiya fujo kama hizi zisitokea tena katika Visiwa vya Zanzibar ambavyo huzoretesha shughuli za Kitalii ikizingatiwa wakati huu ni msimu wa Utalii ikizingatiwa Zanzibar ni moja ya nchi zilizokuwa na Vivutio vya Utalii.  



SHEKH. Saleh Zam, akitowa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya za Kiislam Zanzibar baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. (chanzo: OthamanMapara)