Mkazi wa
Sharifu Shamba, Abdallah Kondo, akitoa duku duku lake kwa Mbunge wa Ilala, Mussa
Azzan 'Zungu', wakati Mbunge huyo, alipofika eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza
matatizo ya wapiga kura wake na kuzungumza nao jijini leo. (Picha zote na Kassim
Mbarouk)
Baadhi ya
wakazi wa Sharif Shamba, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na
baadhi yao kuhusu matatizo yanayowakabili kwenye eneo lao hilo, mbele ya Mbunge
wao, Mussa Zungu, wakati alipowatembelea kusikiliza matatizo yao
leo.
Mbunge wa
Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', (wa pili kushoto), akiwa na Diwani wa Kata ya Ilala,
Edson Fungo (wa tatu) na Mwenyekiti wa mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah,
wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wakazi wa mtaa huo,
wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wapiga kura wake
na kuzungumza nao jijini leo.
Mkazi wa
Sharif Shamba, Ilala jijini Dar es Salaam, Mariam Mkupama, akitoa baadhi ya
kero zinzowakabili mtaani hapo kwa Mbunge wao Mussa Zungu, alipokuwa akisikiliza
matatizo yao yanayowakabili mtaani hapo leo.
Baadhi ya
wakazi hao wakiwa katika mkutano huo leo, wakisikiliza masuala mbalimbali
yaliyokuwa yakitolewa na baadhi yao kwa Mbunge wao Mussa Azzan Zungu, alipofika
mtaani hapo kusikiliza matatizo yao na kuzungumza nao.
Mbunge wa
Ilala, Mussa Zungu (wa pili kushoto), akiwa na uongozi wa Kata ya Ilala na
wa mtaa wa Sharif Shamba, akinakili matatizo na hoja mbalimbali zilizokuwa
zikitolewa na kuwasilishwa kwake na wakazi wa Sharif Shamba, wakati alipokwenda
kusikiliza matatizo yao pamoja na kuzungumza nao leo jioni.
Bi. Mtumwa
Abdallah, akitoa matatizo yanayowakabili mtaani hapo mbele ya Mbune wa Ilala,
Mussa Zungu (hayupo pichani), aliyotaja kuwa ni adha ya magari makubwa ambayo
huuingizwa mtaani hapo na kusababisha kukata waya za umeme, hatua inayopelekea
kuikosa nishati hiyo mara kwa mara.
Mbunge wa
Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', (wa pili kushoto), akisoma moja ya barua
aliyokabidhiwa na mmoja wa wakazi wa mtaa wa Sharif Shamba, kuhusiana na njia
mbalimbali alizokuwa akipitia katika kutatua baadhi ya matatizo yao lakini bila
kupata mafaniko yoyote yale. Wa tatu ni Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo,
Mwenyekiti wa mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah (wa kwanza kushoto) na
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mtaa huo, Zadock Munisi, wakiwa
katika mkutano huo.
Baadhi ya
akinamama wakazi wa mtaa wa Sharif Shamba, wakisikiliza hoja mbalimbali
zilizokuwa zikiwasilishwa kwa Mbunge Zungu leo jioni.
Wananchi
wakazi wa mtaa huo, wakimsikiliza Mbunge wao, Mussa Zungu alipokuwa akijibu hoja
zao, walizokuwa wakizitoa kwake na kwa uongozi wa Kata na mtaa wao
huo.
Mbunge wa
Ilala, Mussa Zungu akizungumza na wakazi wa mtaa wa Sharif Shamba mara baada ya
kusikiliza hoja na matatizo yao kwenye mkutano wao huo leo
jioni.
Baadhi ya
wakazi wa mtaa huo, wakimsikiliza Mbunge wao, Mussa Zungu, wakati alipokuwa
akizungumza nao kwyenye mkutano huo leo jioni.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah, akijibu baadhi ya tuhuma alizokuwa
ametuhumiwa na kuwasilishwa kwa mbunge Zungu (kulia), kwenye mkutao
huo.
Mbunge wa
Ilala, Mussa Zungu (katikati), Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo (kulia) na
Mwenyekiti wa mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah (kushoto), wakisikiliza maelezo
mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa kwa awamu ya pili na wakazi wa Sharif Shamba
kwenye mkutano huo leo jioni.
Mkazi wa
mtaa huo, Sakina Juma, akiwasilisha kwa Mbunge Zungu kilio chao, mtaani hapo,
ikiwemo tatizo la maji na kuaharibika kwa pumpu ya kisima chao kirefu cha maji
wanayotumia mtaani hapo, ambapo katika jibu lake Mbunge Zungu aliahidi
kushughulikia tatizo hilo haraka ikiwemo kutoa tenki la kuhifadhia maji ya
matumizi ya mtaa huo.
No comments:
Post a Comment