Thursday, June 28, 2012

LIONS CLUB YACHIMBISHA VISIMA SHULE ZA MSINGI MINAZI MIREFU NA AIRWING KIPAWA JIJINI DAR

Diwani wa Kata ya Kipawa Bonah Kaluwa, akifungua moja ya bomba la maji ya kisima walichokabidhiwa na wahisani hao katika Shule ya Msingi ya Airwing Kipawa. Diwani Kaluwa ndiye aliyefanikisha mpango wa upatikanaji wa visima hivyo kupitia Lions Club.
Gavana wa Lions Club Internation Tanzania na Uganda, Satish Sherma, akitoa hotuba fupi kabla ya kukabidhi visima hivyo.
Gavana wa Lions Club Internation Tanzania na Uganda, Satish Sherma, akimvalisha beji ya Lions Club, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa wakati wa makabidhiano ya visima hivyo.
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (wa pili kulia), akizungumza jambo na Gavana wa Lions Club Internation Tanzania na Uganda, Satish Sherma (kushoto) na Katibu Mkuu wa Lions Club, Mustafa Kundrat.
Wanafunzi wa Shule za Minazi Mirefu na Airwing wakipiga makofi wakati wa kukabidhiwa visima hivyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Minazi Mirefu, Daniel Mwamakula (kulia), akitoa neno la shukurani kwa wahisani hao na wageni waalikwa.
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kulia), akimkabidhi fedha Bakari Ally ambaye alikuwa msimamizi wa ujenzi wa visima hivyo.

YANGA SPORTS YAFANYA MAZOEZI KUJIFUA KAGAME CUP

Kifaa kipya cha Yanga, kutoka Simba Kelvi Yondani, akipiga mpira wakati wa mazoezi ya timu hiyo kujifua kwa ajili ya kujiweka sawa na mashindano ya Kombe la Kagame, mashindano yatakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji mpya wa Yanga, Simon Msuva (mbele), akiwaongoza wenzake katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye fukwe za Coco Beach jijini Dar es Salaam jana. Wanaomfuatia ni beki mpya wa klabu hiyo, Kelvin Yondani na Godfrey Taita. (Picha zote na Mpiga Picha wa Habari Mseto Blog).
Nurdin Bakari akijifua wakati wa mazoezi hayo jana.
Nizar Khalfan (kushoto), akijifua na wachezaji wenzake wa Yanga katika mazoezi hayo.
Mmoja wa wachezaji wapya wa Yanga akiwa kwenye mazoezi hayo.

Wachezaji wa Yanga wakikimbia katika mazoezi mepesi ya kujiandaa na mashindano ya Kagame Cup yanayotarajiwa kuanza Julai 14 jijini Dar es Salaam.
Nizar Khalfan akiwa katika mazoezi na timu yake mpya ya Yanga katika ufukwe wa Coco Beach Oysterbay jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa Yanga wakipiga danadana, wakati wa mazoezi yao kwenye ufukwe wa Coco Beach, jijini Dar es Salaam leo.

NYOTA WA NIGERIA OMOTOLA JALADE ATEMBELEA YATIMA JIJINI DAR

<><> <><> <><>
Mchezaji wa Filamu kutoka nchini Naigeria Omotola Jalade katikati akiwa katika picha ya pamoja na mwigizaji Wema Sepetu (kushoto) na Khadija Mwanamboka pamoja na watoto yatima wa kituo cha Tanzania Mitindo House cha jijini Dar es Salaam leo. Omotola amekuja nchini maalum kwa ajili ya uzinduzi wa filamu ya Wema Sepetu Super Star ambayo imezinduliwa jana kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam.


Omotola Jalade akiwasili kituoni hapo leo.

Omotola Jalade na Wema Sepetu wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo cha Tanzania Mitindo House.

MBUNGE ZUNGU (ILALA) AKUTANA NA WAKAZI WA SHARIF SHAMBA JIJINI DAR

Mkazi wa Sharifu Shamba, Abdallah Kondo, akitoa duku duku lake kwa Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', wakati Mbunge huyo, alipofika eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wapiga kura wake na kuzungumza nao jijini leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya wakazi wa Sharif Shamba, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na baadhi yao kuhusu matatizo yanayowakabili kwenye eneo lao hilo, mbele ya Mbunge wao, Mussa Zungu, wakati alipowatembelea kusikiliza matatizo yao leo.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', (wa pili kushoto), akiwa na Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo (wa tatu) na Mwenyekiti wa mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na wakazi wa mtaa huo, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kusikiliza matatizo ya wapiga kura wake na kuzungumza nao jijini leo.
Mkazi wa Sharif Shamba, Ilala jijini Dar es Salaam, Mariam Mkupama, akitoa baadhi ya kero zinzowakabili mtaani hapo kwa Mbunge wao Mussa Zungu, alipokuwa akisikiliza matatizo yao yanayowakabili mtaani hapo leo.
Baadhi ya wakazi hao wakiwa katika mkutano huo leo, wakisikiliza masuala mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na baadhi yao kwa Mbunge wao Mussa Azzan Zungu, alipofika mtaani hapo kusikiliza matatizo yao na kuzungumza nao.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (wa pili kushoto), akiwa na uongozi wa Kata ya Ilala na wa mtaa wa Sharif Shamba, akinakili matatizo na hoja mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na kuwasilishwa kwake na wakazi wa Sharif Shamba, wakati alipokwenda kusikiliza matatizo yao pamoja na kuzungumza nao leo jioni.
Bi. Mtumwa Abdallah, akitoa matatizo yanayowakabili mtaani hapo mbele ya Mbune wa Ilala, Mussa Zungu (hayupo pichani), aliyotaja kuwa ni adha ya magari makubwa ambayo huuingizwa mtaani hapo na kusababisha kukata waya za umeme, hatua inayopelekea kuikosa nishati hiyo mara kwa mara.
Mbunge wa Ilala, Mussa Azzan 'Zungu', (wa pili kushoto), akisoma moja ya barua aliyokabidhiwa na mmoja wa wakazi wa mtaa wa Sharif Shamba, kuhusiana na njia mbalimbali alizokuwa akipitia katika kutatua baadhi ya matatizo yao lakini bila kupata mafaniko yoyote yale. Wa tatu ni Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo, Mwenyekiti wa mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah (wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wa mtaa huo, Zadock Munisi, wakiwa katika mkutano huo.
Baadhi ya akinamama wakazi wa mtaa wa Sharif Shamba, wakisikiliza hoja mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwa Mbunge Zungu leo jioni.
Wananchi wakazi wa mtaa huo, wakimsikiliza Mbunge wao, Mussa Zungu alipokuwa akijibu hoja zao, walizokuwa wakizitoa kwake na kwa uongozi wa Kata na mtaa wao huo.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu akizungumza na wakazi wa mtaa wa Sharif Shamba mara baada ya kusikiliza hoja na matatizo yao kwenye mkutano wao huo leo jioni.
Baadhi ya wakazi wa mtaa huo, wakimsikiliza Mbunge wao, Mussa Zungu, wakati alipokuwa akizungumza nao kwyenye mkutano huo leo jioni.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah, akijibu baadhi ya tuhuma alizokuwa ametuhumiwa na kuwasilishwa kwa mbunge Zungu (kulia), kwenye mkutao huo.
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (katikati), Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo (kulia) na Mwenyekiti wa mtaa wa Sharif Shamba, Mtoro Shah (kushoto), wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa kwa awamu ya pili na wakazi wa Sharif Shamba kwenye mkutano huo leo jioni.
Mkazi wa mtaa huo, Sakina Juma, akiwasilisha kwa Mbunge Zungu kilio chao, mtaani hapo, ikiwemo tatizo la maji na kuaharibika kwa pumpu ya kisima chao kirefu cha maji wanayotumia mtaani hapo, ambapo katika jibu lake Mbunge Zungu aliahidi kushughulikia tatizo hilo haraka ikiwemo kutoa tenki la kuhifadhia maji ya matumizi ya mtaa huo.
Mbunge Mussa Azzan Zungu, akizungumza na wakazi hao wakati alipokuwa akihitimisha mkutano wake na wakazi hao katika kusikiliza matatizo yanayowakabili pamoja na kero mbalimbali mtaani hapo. Wa pili kulia ni Diwani wa Kata ya Ilala, Edson Fungo, Mwnyekiti wa mtaa huo, Mtoro Shah (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM wa tawi la Sharif Shamba, Zadock Munisi

PICHA: MATUKIO BUNGENI


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum, Leticia Nyerere kwenye viwanja vya Bunge, Mjini Dodoma leo Juni 27,2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Mbunge wa Mbinga Mashariki Gaudence Kayombo, kwenye jengo la utawala la Bunge Mjini Dodoma leo Juni 27,2012.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimina na Mbunge wa Dole, Sylvester Mabumba, viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo Juni 27, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wawekezaji katika sekta ya madini mkoani Mara kutoka kampuni ya Gemini Corporation ya Urusi, ofisini kwake Bungeni mjini Dodoma leo Juni 27,2012. Kushoto ni mwenyeji wao , Mbunge wa Viti Maalum Zainab Kawawa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na akinamama wawekezaji katika sekta ya madini, mkoani Mara kutoka Kampuni ya Gemini Corporation ya Urusi mara baada ya mazungumzo yao leo.


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na wawekezaji katika sekta ya madini mkoani Mara kutoka kampuni ya Gemini Corporation ya Urusi baada ya kuzungumza nao, Ofisini kwake Bungeni Mjini Dodoma leo Juni 27,2012. Kushoto ni Mwenyeji wao , Mbunge wa Viti Maalum Zainab Kawawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Fedha, William Mgimwa, akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba, nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.


Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Assumpter Mshamba (CCM), akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, bungeni mjini Dodoma leo.


Mbunge wa Moshi mjini, Phillemon Ndesamburo (Chadema), akisalimiana na mjasiriamali, Emma Kawawa, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe amabye sasa ni marehemu Rashid Mfaume Kawawa, walipokutana kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma leo. Kulia ni Mbinge wa Viti Maalum, Lucy Owenye (Chadema), ambaye ni mtoto wa Ndesamburo.


Waziri Mwakyembe akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma leo.

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Lucy Kiwelu, akichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu bungeni mjini Dodoma leo.
Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA, ambaye ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzania Bungeni, Freeman Mbowe, nje ya Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Wednesday, June 27, 2012

JIHADHARI NA HUU UTAPELI

Kutokana na Kupenda Kuchunguza Mambo hususani ya msingi sana. Niliona Tangazo la Kazi Kupitia moja ya Blogu za Hapa tanzania nilihisi lakini Sikupenda Kuhukumu bila Kuwa na ushahidi na ufahamu wa kutosha kuhusu hilo Swala.

Hilo tangazo lilikua ni La Kazi nikaomba baada ya hapo wakaniambia nitumie CV, na kujibiwa kuwa baada ya Siku Mbili za Kazi nitajibiwa. Niliomba hiyo nafasi wiki iliyopita na Jana Nikajibiwa na Huu hapa Chini Ndio Ujumbe niliotumiwa na Hao Wahuni wa Mtandaoni ..

Habari,

Ninayofuraha kukufahamisha kuwa ombi lako la kufanya kazi na Mercycorps Nicaragua(Central America) limekubaliwa,nimeambatanisha barua ya kukubaliwa ambayo utasaini panapohusika na kuirudisha kwetu.
Kwa mujibu wa sheria za immigration hapa Nicaragua,NGO inatakiwa kukuombea Visa/work permit ili uweze kuja hapa kuanza kazi,kwa sasa hakuna ubalozi wa Nicaragua hapo Tanzania.
Kama ambavyo nilikutaarifu hapo awali unatakiwa kutuma malipo kwa ajili ya kuprocess Visa/Work permit yako mapema kama ambavyo barua ya kukubaliwa kazi inavyojieleza ili kutoa muda mzuri kwa NGO kuprocess kwa wakati ambapo itachukua siku 4 za kazi kupata kibali hicho cha Visa/Work permit.

Sasa katika kurahisisha utumaji wa malipo hayo Management imeomba kutumia account ya mfanyakazi ambaye yeye ana account ambayo ni International Account ambayo benki yake pia inapatikana hapo nchini Tanzania,hii ni kwa sababu ya kurahisisha na kuondoa gharama za utumaji na ucheleweshaji wa kupata malipo kwa wakati.
Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kubadili hiyo dola $197 kuwa Tanzania shillings ambayo ni sawa na Tsh.315,200/- ,harafu utadeposit hiyo Tsh.315,200/- kwenye account ifuatayo;
Tafadhali nakuomba uscan na unitumie payslip/Deposit slip baada ya kufanya malipo kwa Sababu Management itaihitaji kwa sababu za kiofisi,

Bank Name: Stanbic Bank
Account Name: Jacob E.E
Account Number: 0140518946701
Visa Card Number: 4313321007132065

Regards
Lilian Kisanga
Project Manager
Mercycorps
Nicaragua

Kutokana na Ujumbe huo Niliingiwa na Wasiwasi Sana na kujiuliza vitu vifuatavyo: Iweje Swala la Kulipa pesa ya Visa/Work Permit niliambiwa ni USD 197 iweje sasa Nilipe kwa Tsh? Halafu pili Iweje Nilipe kwenye Account ya Mtu binafsi? Baada ya hapo Ikabidi nifuatilie kuhusu hii account ikanibidi niwasiliane na Stanbic Bank kwaajili ya Ufafanuzi zaidi na Ubalozi wa Marekani.Huu hapa Chini ni Ujumbe niliopokea Kutoka Benki ya Stanbic Bank.....unasomeka hivi
"
Habari ,
Unashauriwa kwamba kwa sasa usiweke hela yoyote kwenye hiyo akaunti ya Jacob E.E.
Salamu,
Patricia
"
Ndugu Zangu Huu Ni Utapeli Kwahiyo Msitume

KOVA AZUNGUMZIA UTEKAJI WA DR. ULIMBOKA


Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio la utekaji nyara na kujeruhi lililompata kiongozi mgomo wa Madaktari Steven Ulimboka anayedaiwa kutekwa na watu watano wakati akipata kinwaji katika klabu ya Leaders Kiondoni jijini Dar es salaam.
Waandishi wa habari waimsikilza kamanda Suleiman Kova katika kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es salaam leo mchana.
Kamanda Kova amesema Ulimboka aliokotwa na msamaria mwema ambaye hakutaka kumtaja jina lake kiusalama na kutoharibu upelelezo kuwa msamaria mwema huyo alimuokota Ulimboka katika msitu wa Mabwepande na kutoa taarifa kituo cha polisi cha Bunju, ambapo polisi aliyekuwa zamu alichukua maelezo yake na baadae Steven Ulimboka kuletwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Kamanda Kova amesema jeshi la Polisi Kanda Maalum limeunda jopo maalum kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi wa tukio hilo la utekaji nyara, kwani ni tukio la kwanza kutokea nchini, ameongeza kwamba wahusika wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo watachukuliwa hatua za kisheria na sheria itafuata mkondo wake ili kukomesha matukio mengine kama hayo

Kamati Ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Chini Ya Mwenyekiti Wake Edward Lowassa Yaanza Ziara ya Siku 14 katika Balozi za Tanzania Kwenye nchi za Marekani,Canada,Uingereza na Asia Kukagua Namna Zinavyotekeleza Mambo ya Sera na Uchumi


Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, muda mfupi kabla ya wajumbe wa kamati hiyo kuelekea nchini Canada, Marekani na Uingereza kwa ziara ya kujifunza.

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo.Picha Zote na Mpiga Picha Maalum wa Francis Dande